BAR


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Monday, 23 April 2018

KUELEKEA SHEREHE ZA MUUNGANO.


Katika kuelekea maadhimisho ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar(Tanzania) yatakayo fanyika katika Mkoa wa Dododoma tarehe 26/04/2018, Baraza la Vijana Zanzibar liliandaa Kongamano la sherehe za Muungano lililo fanyika siku ya Jumapili tarehe 22/04/2018 Wilaya ya Kaskazi B eneo la Kiwengwa katika ukumbi wa Hotel ya Spano,kongamano hilo lilijadili mada mbili kuu ambazo ni:
i)Faida za Muungano.
ii)Maendeleo ya Baraza la Vijana. 
Hivyo vijana kutoka Shehia na wilaya zote za Unguja waliweza kushiriki na kutoa michango yao vyema ili kufanikisha sherehe hizo.
Mgeni rasmi katika sherehe za Kongamano hilo alikua ni mkuu wa Wilaya ya kaskazini B Mheshmiwa Rajab Ali Rajab.
Aidha nae Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo mhesmiwa Amour Hamil Bakar alihudhuria katika kongamano hilo ili kuwapa nguvu Vijana pia kuwajenga kifikra juu ya uzalendo wa nchi yao.

No comments:

Post a Comment