Baraza la Viajana Zanzibar
limefanya kikao cha Baraza la Watendaji na
kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kufanya Tathmini ya Program ya Ajira kwa
Vijana na maendeleo yake kwa Vijana,pia limejadili namna ya kuongeza ushiriki
wa Vijana kupitia Mabaraza ya Vijana Wilaya na Shehia na kuzungumzia namna ya
matumizi sahihi ya usafiri wa Mabaraza ya Vijana Wilaya .
Akizungumza na wajumbe wa kikao
hicho Siku ya ijuma tarehe 03/01/2020 Mwenyekiti wa Baraza la Vijana
Zanzibar ndugu Khamis Rashid Kheir aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kwa kuendelea kuwasaidia Vijana kwa kuanzisha Program ya Ajira ya kwa
Vijana ambayo imeanza kuleta faida kwa Vijana.
No comments:
Post a Comment