BAR


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Monday, 30 March 2020

BARAZA LA VIJANA ZANZIBAR LAGAWA VIFAA KINGA.



Baraza la Vijana Zanzibar limetoa mikakati yao juu ya kupambana na maradhi ya corona yanayosababishwa na kirusi cha COVID-19 ambapo wameshaanza kuwaagiza na kuwashauri vijana wao kufuata maelekezo yote yanayotolewa na Serikali yao pamoja na kusambaza taarifa zilizosahihi na zilizothibitishwa na Serikali yao, pia Baraza hilo limewakabidhi vifaa vya kujikinga na maradhi hayo ikiwemo ndoo za maji ya kunawia, sabuni na saniter

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana zanzibar ndugu Khamis Rashid Kheir (makoti) amegawa vifaa hivyo kila wilaya kwa kuanzia na Wilaya 7 za Unguja na baadae watatoa vifaa kwa Wilaya 4 za Pemba

Kwaupande wao Vijana walioshiriki mkutano huo wamepongeza jitihada za Baraza la Vijana zanzibar katika kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kudhibiti ugonjwa huo ambao ni tishio duniani kote.

Imetolewa:
Baraza la Vijana Zanzibar
30/03/2020

Thursday, 26 March 2020

BARAZA LA VIJANA ZANZIBAR LAZUNGUMZIA KORONA.

Baraza la Vijana Zanzibar Leo asubuhi limefanya kipindi cha live cha Tuongee na ZBC kwa ajili ya kuzungumzia juu ya suala la maradhi ya corona na namna vijana tulivyojipanga kukabiliana na tatizo hilo hapa nchini kwetu.
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar ndugu Khamis R. Kheir  (MAKOTI ) na Mwenyekiti wa kamati ya Afya ya Baraza la Vijana Dr. Ali Sinyori  (MD) Wamewataka Vijana kuchukua Tahadhari na hatua za Makusudi za kujikinga na Ugonjwa huu hatari ambao kwa sasa umekua Ni janga la Kimataifa .

Monday, 3 February 2020

BARAZA LA VIJANA ZANZIBAR LAFANYA KIKAO NA SMIDA .



Baraza la Vijana Zanzibar lafanya kikao na Taasisi ya SMIDA iliyopo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara ambayo ina jukumu la kusimamia na kukuza Viwanda vidogo vidogo.
Kikao hicho kimefanyika leo Jumatatu tarehe 03/02/2020 katika  ofisi ya Baraza la Vijana Zanzibar Mwanakwerekwe Unguja.
Akiwakaribisha Viongozi wa SMIDA na wajumbe wengine waalikwa walio hudhuria katika kikao hicho Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar ndugu Khamis R. Kheir alisema wamekubaliana na SMIDA kwanza kukutana na Viongozi wa Vijana Unguja na Pemba ili kuwaelewesha namna ya kuweza kuwezeshwa ili kujikomboa kiuchumi kwani Serikali ya SMZ imejipanga kuwawezesha wananchi wakiwemo Vijana kwa kuwapatia Mikopo ambayo wataendeleza shughuli zao ikiwemo shughuli za Mwani, Madagaa, Chumvi na Miradi ya maziwa.

Nae  Mkurugenzi Mkuu wa SMIDA Dr Haji Abdulhamid   ametoa malezo ya ufafanuzi wa fursa zilizopo  pamoja na  upatikanaji wa fedha za KHALIFA FUNDS kwa njia ya mikopo  amewataka Vijana kuchangamkia fursa na kuhakikisha wanajipanga vizuri ili kuweza kuwezeshwa kupitia Mfuko wa SMIDA kupitia KHALIFA FUNDS.

Imetolewa;
Baraza la Vijana Zanzibar.
03/02/2020

Thursday, 30 January 2020

MAKOTI AENDELEA KUMTAMBULISHA

# KAZI INAENDELEA

Mwenyekiti  wa Baraza la Vijana Zanzibar  ndugu Khamis R. Kheir ( MAKOTI ) aendelea kumtambulisha kwa Viongozi mbali mbali wa Serikali,  Vijana na  wanafunzi wa Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la  Vijana la Tanzania Red Cross Society ndugu Rahim Kalyango. Amemtambulisha kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mh. Ayoub Mohammed Mahmoud, Skuli ya Sekondari Haileselaasie, Chuo Cha Afya Mbweni Zanzibar.
Mwenyekiti amefanya hivyo ili kujenga ushirikiano Mwema na TRCS kwani Vijana lazima washikamane kufikia maendeleo ya kweli.

Imetolewa;
Baraza la Vijana Zanzibar.
29/01/2020

Monday, 6 January 2020

BARAZA LA VIJANA ZANZIBAR LAFANYA KIKAO NA BARAZA WATENDAJI ZANZIBAR.


Baraza la Viajana Zanzibar limefanya kikao cha Baraza la Watendaji  na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kufanya Tathmini ya Program ya Ajira kwa Vijana na maendeleo yake kwa Vijana,pia limejadili namna ya kuongeza ushiriki wa Vijana kupitia Mabaraza ya Vijana Wilaya na Shehia na kuzungumzia namna ya matumizi sahihi ya usafiri wa Mabaraza ya Vijana Wilaya  .
Akizungumza na wajumbe wa kikao hicho  Siku ya ijuma tarehe 03/01/2020 Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar ndugu Khamis Rashid Kheir aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuendelea kuwasaidia Vijana kwa kuanzisha Program ya Ajira ya kwa Vijana ambayo imeanza kuleta faida kwa Vijana.

Thursday, 5 December 2019

BARAZA LA VIJANA ZANZIBAR LAKABIDHIWA PIKIPIKI



Baraza  la Vijana Zanzibar lakabidhiwa vyombo vya usafiri (Pikipiki aina ya Boxer) kwa ajili ya kurahisisha shughuli zao za kazi .Jumla ya Pikipiki 12 zimekabidhiwa Mabaraza ya Vijana Wilaya na Taifa na Mwenyekiti wa Baraza la  Vijana Zanzibar ndugu Khamis Rashid Kheir amepokea Pikipiki hizo siku ya Alkhamis tarehe 5/12/2019 kutoka kwa Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Balozi Ali Karume
Zoezi hilolimeshuhudiwa na Viongozi wa Wizara ,Wenyeviti wa Mabaraza ya Vijana

Monday, 2 December 2019

PROGRAM YA AJIRA KWA VIJANA

Mkurugez Vijana wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo ndugu Mwanaidi Mohamed Ali akizungumza na Vijana wa Mabaraza ya Vijana kutoka Wilaya zote za Unguja ambao wataanza mafunzo ya Ushoni , Fundi chuma (Welding) pamoja na uchongaji. Mafunzo hayo yataanza siku ya Jumatatu tarehe 02/12/2019 katika chuo cha Mafunzo Vikokotoni Zanzibar.
kikao hicho kilicho fanyika siku ya jumanne tarehe 26/11/2019 katika ukumbi wa Eqwip Hubs uliopo Mwanakwerekwe kilikua na lengo la kutoa muongozo kwa vijana hao waliobahatika kupata fursa hizo za mafunzo