BAR


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Tuesday, 8 June 2021


 Mwenyeki wa Baraza la Vijana Zanzibar ndugu Yunus Juma Ali akila kiapo cha uadilifu  kuliongoza Baraza laVijana  Zanzibar baaa ya kushinda uchaguzi  kwa nafasi ya Mwenyekiti  


 Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana Zanzibar ndugu Salum Issa Ameir akitumbukiza kura yake katika kisanduguku cha kura katika uchaguzi mkuu wa Baraza la Vijana Zanzibar


 Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana Zanzibar ndugu Salum Issa Ameir akipokea karatasi ya kura katika uchaguzi mkuu wa Baraza la Vijana Zanzibar 


Baraza la vijana Zanzibar limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kufanikisha zoezi la uchaguzi wa Baraza la vijana Taifa siku ya Tarehe 30/05/2021 pamoja na mkutano mkuu uliofanyika Tarehe 31/05/2021. Kwa upande wa uchaguzi zoezi lilifanikiwa vizuri na matokeo yalikuwa kama ifuatavyo
NAFASI YA MWENYEKITI
Alieshinda ni
Ndugu: YUNUS JUMA ALI
NAFASI YA MAKAMO MWENYEKITI
Alieshinda ni
Ndugu: RUSHDA KHAMIS KASSIM
Na kwaupande wa washindi wa baraza la watendaji ni kama ifuatavyo
1.JAMILA BORAFIA HAMZA
2. HASINA YUSSUF JUMA
3. AMINA MIRAJ HASSAN
4. MUSSA SULEIMAN MGENI
5. MASOUD MUHAMED ISSA
6. RASHID MUHAMED OTHMAN
7. FARID MUHAMED HAJI
Baraza la vijana Zanzibar linawapongeza washindi wote na linawataka kufanya kazi kwa bidii kama ambavyo sheria na kanuni za Baraza zinavyoongoza
Ahsanteni sana
Imetolewa na Kitengo cha Habar na Mawasiliano
Baraza la vijana zanzibar.

 

Friday, 26 February 2021



Baadhi wajumbe wa kamati ya Uchaguzi wa Baraza la Vijana Zanzibar wakisaini kiapo cha kuwa mjumbe wa kamati ya kusimamia uchaguzi wa Baraza la Vijana Zanzibar .
 

 





Waziri wa Habari ,Vijana Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Tabia Maulid Mwita akiwaapisha wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi Taifa ambayo imepewa jukumu la kusimamia Uchaguzi wa Baraza la Vijana Zanzibar katika ngazi ya wilaya na Taifa.
Zoezi hili la kuwwapisha wajumbe wa kamati ya uchaguzi Taifa limefanyika katika Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo iliyopo Migombani siku ya Jumatatu tarehe 23/02/2021.
Aidha Mheshimiwa Waziri aliwataka wajumbe hao wa kamati ya kusimamia Uchaguzi kuwa waadilifu ili waweze kuendesha uchaguzi kwa misingi ya Huru na Haki

Thursday, 7 May 2020

MMWEKITI WA BARAZA LA VIJANA AKIGAWA NGUO

Baraza la Vijana Zanzibar limeendelea na zoezi  la kusaidiai jamii kwa kuwapatia baadhi ya wananchi nguo    ambazo zitawasaidia wananchi na hasa Vijijini. Akikabidhi nguo hizo Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar ndugu Khamis R. Kheir ( MAKOTI) kwa Mzee Kassim Makame kutoka Wilaya ya Kaskazini A kwa ajili ya kuwapatia familia  ( kaya ) ambazo zenye mahitaji.

Mwenyekiti  huyo amesema Programu hiyo ya kugawa nguo Vijijini ilifanywa na Baraza la Vijana kushirikiana na Vijana wazalendo kabla ya ya kuibuka kwa maradhi ya Corona nchini.  Pia Mwenyekiti anawaomba watu au mashirika yenye uwezo kushirikiana na Baraza hilo au wenyewe kuwasaidia wananchi wenye mahitaji katika kipindi hichi na hasa wakati wa sikukuu.

Imetolewa;
Baraza la vijana Zanzibar.