Waziri wa Habari ,Vijana Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Tabia Maulid Mwita akiwaapisha wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi Taifa ambayo imepewa jukumu la kusimamia Uchaguzi wa Baraza la Vijana Zanzibar katika ngazi ya wilaya na Taifa.
Zoezi hili la kuwwapisha wajumbe wa kamati ya uchaguzi Taifa limefanyika katika Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo iliyopo Migombani siku ya Jumatatu tarehe 23/02/2021.
Aidha Mheshimiwa Waziri aliwataka wajumbe hao wa kamati ya kusimamia Uchaguzi kuwa waadilifu ili waweze kuendesha uchaguzi kwa misingi ya Huru na Haki
No comments:
Post a Comment