BAR


Blogger Tips and TricksLatest Tips And TricksBlogger Tricks

Thursday, 7 May 2020

MMWEKITI WA BARAZA LA VIJANA AKIGAWA NGUO

Baraza la Vijana Zanzibar limeendelea na zoezi  la kusaidiai jamii kwa kuwapatia baadhi ya wananchi nguo    ambazo zitawasaidia wananchi na hasa Vijijini. Akikabidhi nguo hizo Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar ndugu Khamis R. Kheir ( MAKOTI) kwa Mzee Kassim Makame kutoka Wilaya ya Kaskazini A kwa ajili ya kuwapatia familia  ( kaya ) ambazo zenye mahitaji.

Mwenyekiti  huyo amesema Programu hiyo ya kugawa nguo Vijijini ilifanywa na Baraza la Vijana kushirikiana na Vijana wazalendo kabla ya ya kuibuka kwa maradhi ya Corona nchini.  Pia Mwenyekiti anawaomba watu au mashirika yenye uwezo kushirikiana na Baraza hilo au wenyewe kuwasaidia wananchi wenye mahitaji katika kipindi hichi na hasa wakati wa sikukuu.

Imetolewa;
Baraza la vijana Zanzibar.

No comments:

Post a Comment