Tuesday, 8 June 2021
Baraza la vijana Zanzibar limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kufanikisha zoezi la uchaguzi wa Baraza la vijana Taifa siku ya Tarehe 30/05/2021 pamoja na mkutano mkuu uliofanyika Tarehe 31/05/2021. Kwa upande wa uchaguzi zoezi lilifanikiwa vizuri na matokeo yalikuwa kama ifuatavyo
NAFASI YA MWENYEKITI
Alieshinda ni
Ndugu: YUNUS JUMA ALI
NAFASI YA MAKAMO MWENYEKITI
Alieshinda ni
Ndugu: RUSHDA KHAMIS KASSIM
Na kwaupande wa washindi wa baraza la watendaji ni kama ifuatavyo
1.JAMILA BORAFIA HAMZA
2. HASINA YUSSUF JUMA
3. AMINA MIRAJ HASSAN
4. MUSSA SULEIMAN MGENI
5. MASOUD MUHAMED ISSA
6. RASHID MUHAMED OTHMAN
7. FARID MUHAMED HAJI
Baraza la vijana Zanzibar linawapongeza washindi wote na linawataka kufanya kazi kwa bidii kama ambavyo sheria na kanuni za Baraza zinavyoongoza
Ahsanteni sana
Imetolewa na Kitengo cha Habar na Mawasiliano
Baraza la vijana zanzibar.
Friday, 26 February 2021
Waziri wa Habari ,Vijana Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Tabia Maulid Mwita akiwaapisha wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi Taifa ambayo imepewa jukumu la kusimamia Uchaguzi wa Baraza la Vijana Zanzibar katika ngazi ya wilaya na Taifa.
Zoezi hili la kuwwapisha wajumbe wa kamati ya uchaguzi Taifa limefanyika katika Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo iliyopo Migombani siku ya Jumatatu tarehe 23/02/2021.
Aidha Mheshimiwa Waziri aliwataka wajumbe hao wa kamati ya kusimamia Uchaguzi kuwa waadilifu ili waweze kuendesha uchaguzi kwa misingi ya Huru na Haki
Thursday, 7 May 2020
MMWEKITI WA BARAZA LA VIJANA AKIGAWA NGUO
Baraza la Vijana Zanzibar limeendelea na zoezi la kusaidiai jamii kwa kuwapatia baadhi ya wananchi nguo ambazo zitawasaidia wananchi na hasa Vijijini. Akikabidhi nguo hizo Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar ndugu Khamis R. Kheir ( MAKOTI) kwa Mzee Kassim Makame kutoka Wilaya ya Kaskazini A kwa ajili ya kuwapatia familia ( kaya ) ambazo zenye mahitaji.
Mwenyekiti huyo amesema Programu hiyo ya kugawa nguo Vijijini ilifanywa na Baraza la Vijana kushirikiana na Vijana wazalendo kabla ya ya kuibuka kwa maradhi ya Corona nchini. Pia Mwenyekiti anawaomba watu au mashirika yenye uwezo kushirikiana na Baraza hilo au wenyewe kuwasaidia wananchi wenye mahitaji katika kipindi hichi na hasa wakati wa sikukuu.
Imetolewa;
Baraza la vijana Zanzibar.
Mwenyekiti huyo amesema Programu hiyo ya kugawa nguo Vijijini ilifanywa na Baraza la Vijana kushirikiana na Vijana wazalendo kabla ya ya kuibuka kwa maradhi ya Corona nchini. Pia Mwenyekiti anawaomba watu au mashirika yenye uwezo kushirikiana na Baraza hilo au wenyewe kuwasaidia wananchi wenye mahitaji katika kipindi hichi na hasa wakati wa sikukuu.
Imetolewa;
Baraza la vijana Zanzibar.
Monday, 30 March 2020
BARAZA LA VIJANA ZANZIBAR LAGAWA VIFAA KINGA.
Baraza la Vijana Zanzibar limetoa mikakati yao juu ya kupambana na maradhi ya corona yanayosababishwa na kirusi cha COVID-19 ambapo wameshaanza kuwaagiza na kuwashauri vijana wao kufuata maelekezo yote yanayotolewa na Serikali yao pamoja na kusambaza taarifa zilizosahihi na zilizothibitishwa na Serikali yao, pia Baraza hilo limewakabidhi vifaa vya kujikinga na maradhi hayo ikiwemo ndoo za maji ya kunawia, sabuni na saniter
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana zanzibar ndugu Khamis Rashid Kheir (makoti) amegawa vifaa hivyo kila wilaya kwa kuanzia na Wilaya 7 za Unguja na baadae watatoa vifaa kwa Wilaya 4 za Pemba
Kwaupande wao Vijana walioshiriki mkutano huo wamepongeza jitihada za Baraza la Vijana zanzibar katika kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kudhibiti ugonjwa huo ambao ni tishio duniani kote.
Imetolewa:
Baraza la Vijana Zanzibar
30/03/2020
Thursday, 26 March 2020
BARAZA LA VIJANA ZANZIBAR LAZUNGUMZIA KORONA.
Baraza la Vijana Zanzibar Leo asubuhi limefanya kipindi cha live cha Tuongee na ZBC kwa ajili ya kuzungumzia juu ya suala la maradhi ya corona na namna vijana tulivyojipanga kukabiliana na tatizo hilo hapa nchini kwetu.
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar ndugu Khamis R. Kheir (MAKOTI ) na Mwenyekiti wa kamati ya Afya ya Baraza la Vijana Dr. Ali Sinyori (MD) Wamewataka Vijana kuchukua Tahadhari na hatua za Makusudi za kujikinga na Ugonjwa huu hatari ambao kwa sasa umekua Ni janga la Kimataifa .
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar ndugu Khamis R. Kheir (MAKOTI ) na Mwenyekiti wa kamati ya Afya ya Baraza la Vijana Dr. Ali Sinyori (MD) Wamewataka Vijana kuchukua Tahadhari na hatua za Makusudi za kujikinga na Ugonjwa huu hatari ambao kwa sasa umekua Ni janga la Kimataifa .
Monday, 3 February 2020
BARAZA LA VIJANA ZANZIBAR LAFANYA KIKAO NA SMIDA .
Baraza la Vijana Zanzibar lafanya kikao na Taasisi ya SMIDA iliyopo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara ambayo ina jukumu la kusimamia na kukuza Viwanda vidogo vidogo.
Kikao hicho kimefanyika leo Jumatatu tarehe 03/02/2020 katika ofisi ya Baraza la Vijana Zanzibar Mwanakwerekwe Unguja.
Akiwakaribisha Viongozi wa SMIDA na wajumbe wengine waalikwa walio hudhuria katika kikao hicho Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar ndugu Khamis R. Kheir alisema wamekubaliana na SMIDA kwanza kukutana na Viongozi wa Vijana Unguja na Pemba ili kuwaelewesha namna ya kuweza kuwezeshwa ili kujikomboa kiuchumi kwani Serikali ya SMZ imejipanga kuwawezesha wananchi wakiwemo Vijana kwa kuwapatia Mikopo ambayo wataendeleza shughuli zao ikiwemo shughuli za Mwani, Madagaa, Chumvi na Miradi ya maziwa.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa SMIDA Dr Haji Abdulhamid ametoa malezo ya ufafanuzi wa fursa zilizopo pamoja na upatikanaji wa fedha za KHALIFA FUNDS kwa njia ya mikopo amewataka Vijana kuchangamkia fursa na kuhakikisha wanajipanga vizuri ili kuweza kuwezeshwa kupitia Mfuko wa SMIDA kupitia KHALIFA FUNDS.
Imetolewa;
Baraza la Vijana Zanzibar.
03/02/2020
Thursday, 30 January 2020
MAKOTI AENDELEA KUMTAMBULISHA
# KAZI INAENDELEA
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar ndugu Khamis R. Kheir ( MAKOTI ) aendelea kumtambulisha kwa Viongozi mbali mbali wa Serikali, Vijana na wanafunzi wa Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Tanzania Red Cross Society ndugu Rahim Kalyango. Amemtambulisha kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mh. Ayoub Mohammed Mahmoud, Skuli ya Sekondari Haileselaasie, Chuo Cha Afya Mbweni Zanzibar.
Mwenyekiti amefanya hivyo ili kujenga ushirikiano Mwema na TRCS kwani Vijana lazima washikamane kufikia maendeleo ya kweli.
Imetolewa;
Baraza la Vijana Zanzibar.
29/01/2020
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar ndugu Khamis R. Kheir ( MAKOTI ) aendelea kumtambulisha kwa Viongozi mbali mbali wa Serikali, Vijana na wanafunzi wa Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Tanzania Red Cross Society ndugu Rahim Kalyango. Amemtambulisha kwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mh. Ayoub Mohammed Mahmoud, Skuli ya Sekondari Haileselaasie, Chuo Cha Afya Mbweni Zanzibar.
Mwenyekiti amefanya hivyo ili kujenga ushirikiano Mwema na TRCS kwani Vijana lazima washikamane kufikia maendeleo ya kweli.
Imetolewa;
Baraza la Vijana Zanzibar.
29/01/2020
Monday, 6 January 2020
BARAZA LA VIJANA ZANZIBAR LAFANYA KIKAO NA BARAZA WATENDAJI ZANZIBAR.
Baraza la Viajana Zanzibar
limefanya kikao cha Baraza la Watendaji na
kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kufanya Tathmini ya Program ya Ajira kwa
Vijana na maendeleo yake kwa Vijana,pia limejadili namna ya kuongeza ushiriki
wa Vijana kupitia Mabaraza ya Vijana Wilaya na Shehia na kuzungumzia namna ya
matumizi sahihi ya usafiri wa Mabaraza ya Vijana Wilaya .
Akizungumza na wajumbe wa kikao
hicho Siku ya ijuma tarehe 03/01/2020 Mwenyekiti wa Baraza la Vijana
Zanzibar ndugu Khamis Rashid Kheir aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kwa kuendelea kuwasaidia Vijana kwa kuanzisha Program ya Ajira ya kwa
Vijana ambayo imeanza kuleta faida kwa Vijana.
Thursday, 5 December 2019
BARAZA LA VIJANA ZANZIBAR LAKABIDHIWA PIKIPIKI
Baraza la Vijana Zanzibar lakabidhiwa vyombo vya usafiri (Pikipiki aina ya Boxer) kwa ajili ya kurahisisha shughuli zao za kazi .Jumla ya Pikipiki 12 zimekabidhiwa Mabaraza ya Vijana Wilaya na Taifa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar ndugu Khamis Rashid Kheir amepokea Pikipiki hizo siku ya Alkhamis tarehe 5/12/2019 kutoka kwa Waziri wa Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Balozi Ali Karume
Zoezi hilolimeshuhudiwa na Viongozi wa Wizara ,Wenyeviti wa Mabaraza ya Vijana
Monday, 2 December 2019
PROGRAM YA AJIRA KWA VIJANA
Mkurugez Vijana wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo ndugu Mwanaidi Mohamed Ali akizungumza na Vijana wa Mabaraza ya Vijana kutoka Wilaya zote za Unguja ambao wataanza mafunzo ya Ushoni , Fundi chuma (Welding) pamoja na uchongaji. Mafunzo hayo yataanza siku ya Jumatatu tarehe 02/12/2019 katika chuo cha Mafunzo Vikokotoni Zanzibar.
kikao hicho kilicho fanyika siku ya jumanne tarehe 26/11/2019 katika ukumbi wa Eqwip Hubs uliopo Mwanakwerekwe kilikua na lengo la kutoa muongozo kwa vijana hao waliobahatika kupata fursa hizo za mafunzo
kikao hicho kilicho fanyika siku ya jumanne tarehe 26/11/2019 katika ukumbi wa Eqwip Hubs uliopo Mwanakwerekwe kilikua na lengo la kutoa muongozo kwa vijana hao waliobahatika kupata fursa hizo za mafunzo
Wednesday, 16 October 2019
AFISA MIPANGO WA BARAZA LA VIJANA ZANZIBAR AKIZUNGUMZA NA VIONGOZI WA MABARAZA YA VIJANA WILAYA NA SHEHIA.
Afisa Mipango wa Baraza la Vijana Zanzibar Ndugu Kheir Hassan Khamis akiwapa muongozo viongozi wa mabaraza ya Vijana wilaya na Shehia waliohudhuria katika mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo Vijana katika masuala ya Stadi za Maisha.
BARAZA LA VIJANA ZANZIBAR LAFANYA MAFUNZO YA SIKU TANO.
MWENYEKITI WA BARAZA LA VIJANA AKIFUNGUA MAFUNZO
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar ndugu Khamis Rashid Kheir akifungua mafunzo ya siku tano yanayolenga kuwajengea uwezo Vijana katika stadi za maisha,mpango wa Biashara pamoja na uwandikaji wa Miradi. mafunzo hayo yaliyoanza siku ya jumatano tarehe 09/10/2019 mpaka tarehe 13/10/2019 katika ukumbi wa Malaria.
Tuesday, 1 October 2019
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Wilaya ya Magharibi "B" ndugu Hassan Ali Nassoro akisoma vipengele vya Kanuni ya Baraza la Vijana Zanzibar kitika kakao maalum kilichoadaliwa kwa ajili ya utengenezaji wa kanuni ya Baraza la Vijana suku ya jumamosi tarehe 28/09/2019 katika ukumbi wa mtakwimu mkuu wa serikali uliopo Mazizini Zanzibar.
Subscribe to:
Posts (Atom)
























